Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuachana na benchi lote la ufundi baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa itmu
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo Dk Mshindo Msolla amesema wameamua kuanza upya, hivyo wameachana na benchi lote la ufundi
"Niwaombe radhi waandishi wa habari kwa kuchelewa kuanza mkutano wetu. Kuna masuala muhimu tuhitaji kuyaweka sawa kabla ya kuja kuwataarifu," amesema
"Jambo kubwa tuliowaitia hapa ni moja tu, Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kuachana na benchi lote la ufundi"
"Tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa kocha Mwinyi Zahera, kocha Noel Mwandila na wengine wote waliokuwa kwenye benchi la ufundi"
"Uamuzi huu tumeuchukua ili tuweze kuunda benchi jipya la ufundi. Yawezekana baadhi wanaweza kurejeshwa baadae lakini kama watakidhi vigezo"
"Tumefanya mazungumzo na makocha wote wawili, tumefikia makubaliano tuachane salama"