Yanga ni lazima ianze kupiga hesabu ya kusaka mbadala wa Kelvin Yondani ambaye amebakisha muda mfupi wa kucheza soka la ushindani
Alipostaafu Nadir Haroub, beki Abdallah Shaibu 'Ninja' aliandaliwa kuchukua nafasi yake
Hata hivyo Ninja alitimkia Marekani baada ya kupata 'dili' nono zaidi
Bakari Mwamnyeto ni mlinzi wa kutumainiwa wa Coastal Union ambaye anahusishwa na Yanga
Amekuwa na msimu mzuri na kikosi cha Coastal Union kwenye ligi mpaka sasa
Mwamnyeto alicheza vyema mechi ya kusaka tiketi ya michuano ya CHAN nchini Sudan wengi wakimtabiria kufuata nyayo za Yondani
Hata Yondani mwenyewe amekubali uwezo wa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 akiamini anaweza kuchukua nafasi yake
Yondani amefikisha miaka 35, pengine hana zaidi ya misimu miwili ya kuendelea kucheza soka la ushindani
Kwa siku za karibuni amekuwa akikabiliwa na majeruhi ya mara kwa mara
Mkataba wake na kuitumikia Yanga utamalizika mwishoni mwa msimu
Hakuna shaka, muda ukifika atastaafu kwa heshima akiwa Yanga