Zahera hakuifahamu Yanga - Mwalusako

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2019
Zahera hakuifahamu Yanga - Mwalusako

Katibu mkuu wa zamani wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kocha Mwinyi Zahera hakuifahamu vizuri Yanga.

Mwalusako aliyewahi kuichezea Yanga kabla ya kuwa kiongozi alisema alitambua kocha huyo hawezi kudumu Jangwani.

"Hakujua tabia ya watu wa Yanga, kuna wakati alikuwa akizungumzia hadi masuala ya uongozi na kuona kawaida.

"Hakuisoma Yanga ina watu wenye tabia gani, wanahitaji nini na aishi nao vipi.

"Hata kauli yake ya kwamba wachezaji waliosajili Yanga si wa mashindano ya kimataifa haikuwa sahihi kutamka vile"

"Yeye ndiyo alifanya usajili wa wale wachezaji kwa asilimia kubwa, kama hawakuwa wa mashindano ya kimataifa basi aliingiza 'mkenge' klabu katika usajili.

"Katika vitu ambavyo Yanga hawapendi ni kufungwa na ikitokea wamefungwa basi kuwe na sababu iliyojitosheleza hadi kufungwa na si kizembe," alisema Mwalusako.

Aidha Mwalusako amesema kocha Zahera aliwaacha wachezaji kama Kamusoko ambao walikuwa wazuri bila sababu na kuwasajili wachezaji ambao baadhi yao hawajaonyesha kuisadia timu.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’