Kikosi cha Yanga kiko mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc hapo kesho
Nyota wake nane watakosekana kutokana na sababu mbalimbali zaidi wakiwa majeruhi
Mratibu wa Yanga Dismas Ten amesema wachezaji nane hawatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi ambacho kitaikabili Ndanda Fc kesho
Wachezaji hao ni pamoja na Maybin Kalengo, Lamine Moro, Ali Ali, Cleofas Sospeter na Paulo Godfrey ambao wote ni majeruhi
Wengine ni Juma Balinya, Feisal Salum na Abdulaziz Makame 'Bui'
Ten amesema Feisal Salum amepewa ruhusa maalum ya kwenda kumuuguza mzazi wake, na wengine saba wanakosekana kutokana na kuwa majeruhi.
ADVERTISE HERE