Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wameonyesha mwelekeo mzuri jambo linalompa matumaini kuwa watafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda Fc
Akizungumza baada na mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona leo asubuhi, Mkwasa ameeleza kuridhishwa na ari iliyoonyeshwa na wachezaji katika mazoezi hayo
"Wachezaji wanaonekana wana mwelekeo mzuri, wanakuwa wepesi katika kuelewa, nina imani kubwa sana watafanya vizuri. Mengine tutamuachia Mwenye ez Mungu lakini vijana wako vizuri," amesema
Mkwasa pia amewataka wapenzi, mashabiki na Wanachama wa Yanga kusahau yaliyopita na waungane katika kuiunga mkono timu
"Naomba tushirikiane kwa pamoja, tuweke pembeni matatizo yetu, tuungane tusaidie kuisapoti timu, naamini tutakaa kwenye mstari mzuri na kila mmoja atafurahi"
"Kwa wale watakaokuja kutuunga mkono kesho itakuwa vyema lakini wengine pia watuombee dua ili tuweze kufanikisha malengo ya kupata ushindi"