Tutaifanya Yanga iwe timu ya kuogopwa - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2019
Tutaifanya Yanga iwe timu ya kuogopwa - Mkwasa

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema atahakikisha timu hiyo inarejea kucheza staili ya kushambulia muda wote ili kuvuna mabao mengi.

Mkwasa juzi aliiongoza Yanga kuvuna ushindi wa bao 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Nagwanda Sijaona, Mtwara.

Kocha huyo wa mpito alichukua nafasi ya Mkongomani, Mwinyi Zahera aliyetimuliwa katikati ya wiki iliyopita.

Ushindi huo uliifanya Yanga kufikisha pointi 10, baada ya kucheza michezo mitano, ikishinda mitatu, sare mmoja na kupoteza idadi kama hiyo.

Mkwasa ameahidi kurudisha falsafa ya kucheza kwa kushambulia dakika zote

Alisema kikosi hicho kimejipanga kuhakikisha kinashinda michezo yake yote ya kiporo ili kujikusanyia pointi zitakazoweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

"Nashukuru vijana wangu kwa kufuata maelekezo yangu na kufanikisha ushindi katika mchezo huo,japo nilikuwa na muda mchache na timu,lakini vijana walinipa ushirikiano na kufanya tulichopanga.

"Lengo ni kurudisha falsafa yetu ya kucheza kwa kushambulia, wapenzi wetu wamezoea kuiona Yanga ikimnyima raha mpinzani, tutahakikisha tunafanya hivyo ili kurudisha hadhi yetu na kupata mabao mengi zaidi," alisema.

Mkwasa alisema anataka kukifanya kikosi hicho kuwa tishio kwa wapinzani  na kurudi katika mbio za kufukuzia taji la Ligi Kuu Bara walilipoteza misimu miwili iliyopita.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’