Yanga imepata katibu Mkuu baada ya mwaka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Nov 2019
Yanga imepata katibu Mkuu baada ya mwaka

Julai mwaka 2018 Charles Mkwasa alijiuzulu nafasi ya Katibu Mkuu wa Yanga baada ya kupata maradhi ambayo yalimlazimu kwenda nchini India kutibiwa

Tangu wakati huo, Yanga haikuwa na Katibu Mkuu wa kudumu mpaka hapo jana ilipomtangaza rasmi Dk David Ruhago kushika nafasi hiyo

Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja tangu kuondoka kwa Mkwasa, nafasi hiyo imekaimiwa na viongozi watatu tofauti ambao ni Omar Kaya, Dismas Ten na Thabit Kandoro aliyekaimu nafasi hiyo kwa siku 11 tangu Novemba 1, mwaka huu

Ruhago amewahi kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za Yanga katika vipindi tofauti, uteuzi wake ulikuwa ukisubiri kutangazwa tu, kwani alifahamika toka mwezi Septemba akipitishwa sambamba na viongozi wengine wapya ambao walitangazwa wakati huo Hassan Bumbuli (Afisa Habari) na Antonio Nugaz (Msemaji/Afisa Uhamasishaji)

Kama Katibu Mkuu wa Yanga, Ruhago atakuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, atasimamia shughuli zote za kila siku za timu

Miongoni mwa mambo ambayo Wanayanga watapenda kuona anayasimamia na kuyapatia ufumbuzi, ni pamoja na suala linalomhusu beki Andrew Vicent Chikupe ambaye amegoma kujiunga kikosini mpaka alipwe madai yake ya fedha za usajili yanayofikia Milioni 54

Baada ya mvutano wa hapa na pale, Chikupe amepeleka malalamiko yake TFF ambapo inaelezwa Yanga imepewa muda wa kumaliza sintofahamu ya suala hilo kabla ya uamuzi wa mwisho kuchukuliwa na TFF

Lakini pia kuna suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga. Suala hili limezungumzwa sana wakiwemo viongozi wapya ambapo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla ilikuwa moja ya ajenda zake

Hata hivyo bado hakuonekani kuwa na mchakato hata wa awali unaoashiria kuwepo kwa utekelezaji wake

Angalau wakati wa Mkwasa, aliunda Kamati iliyopewa kazi ya kuthaminisha mali za klabu kabla kuingia hatua ya pili ya mchakato

Kama Mtendaji Mkuu, hili ni eneo ambalo Ruhago anaweza kuwa na mchango mkubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’