Balama afurahia ujio wa Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2019
Balama afurahia ujio wa Mkwasa

Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama anaamini ujio wa kocha Charles Mkwasa umeongeza kitu kwenye kikosi cha timu hiyo

Pamoja na kuwa na timu kwa muda mfupi, Balama amesema kasi waliyoanza nayo chini ya Mkwasa ni ishara kuwa watafanya mambo makubwa zaidi mbeleni

"Ujio wake umetuongezea morali, sasa tunaendelea kuzielewa mbinu zake"

"Ni kocha ambaye kila mchezaji anafurahi kufanya nae kazi. Muda mfupi tuliokuwa naye ametuelekeza mambo mengi ya kiufundi. Amekuwa karibu na wachezaji"

"Naamini tutaendelea kufanya vizuri katika michezo yetu," amesema

Mkwasa aliiongoza Yanga kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc uliofanyika mkoani Mtwara na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Atakiongoza tena kikosi cha timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa Novemba 23 katika uwanja wa Uhuru

Anaendelea kuwaandaa vijana wake katika mazoezi ambayo yanafanyika dimba la Uhuru

Balama amenufaika na ujio wa Mkwasa kwani katika mchezo dhidi ya Ndanda alichezeshwa nafasi ya kiungo, nafasi aliyokuwa akicheza wakati yupo Alliance Fc

Wakati Yanga ikinolewa na Zahera, Balama alikuwa akitumika kama mchezaji kiraka akicheza zaidi nafasi za winga na beki wa kulia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’