Tunahitaji kusajili dirisha dogo - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2019
Tunahitaji kusajili dirisha dogo - Mkwasa

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Disemba 16, yakiwa ni mabadiliko tofauti na misimu iliyopita ambapo dirisha lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Disemba 15

Mapema leo, akizungumza baada ya mazoezi ya kikosi chake yaliyofanyika uwanja wa Uhuru, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema watatumia dirisha hilo kuongeza wachezaji wapya kulingana na mahitaji ya timu

Mkwasa ameeleza kubaini mapungufu kadhaa kwenye kikosi chake ambapo amesema wanahitaji kusajili nyota wapya

"Kiukweli kwa muda ambao nimekaa na timu kuna vitu ambavyo nimeviona miongoni mwa hivyo ni kufanya usajili wakati wa dirisha dogo,” amesema

"Bado sijakutana na kuzungumza na viongozi wangu lakini siku si nyingi nitakutana nao na kuwaeleza kuwa tunatakiwa kuongeza wachezaji kulingana na mahitaji ya timu yetu"

"Siwezi kusema wazi timu ina mapungufu maeneo gani kwani sitakiwi kuliweka hili hadharani mpaka hapo nitakapowaambia viongozi wangu"

Hata hivyo Mkwasa amesema kuna mabadiliko anayaona kwenye kikosi chake tangu alipoanza majukumu yake wiki iliyopita

Amesema anaamini timu itaendelea kuimarika na baadae kuwa imara

"Kiujumla mpaka sasa timu inaendelea vizuri kulingana na mazoezi ambayo tumefanya na naamini muda ambavyo unavyozidi kwenda timu itabadilika na kuwa imara zaidi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’