Tunaendelea kuimarika - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2019
Tunaendelea kuimarika - Mkwasa

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union leo katika mchezo wa kirafiki ni matokeo ya kile ambacho wamekuwa wakikifanyia kazi mazoezini

Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, Mkwasa amesema wachezaji wake waliweza kutekeleza kile alichowaelekeza licha ya changamoto kujitokeza kwenye umaliziaji hasa kipindi cha kwanza

"Tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi kwenye kipindi cha kwanza lakini washambuliaji wangu hawakuwa wakijipanga vizuri hivyo kupoteza nafasi hizo"

"Tulikuwa imara katika ulinzi ndio maana umeona hata bao walilofunga Coastal Union lilikuwa la mchezaji wetu kujifunga. Tuliwabana wakashindwa kutengeneza nafasi za wazi"

"Kipindi cha pili niliwaambia wachezaji wangu waongeze presha langoni kwa Coastal Union, tulitengeneza nafasi nyingi baadhi tumeweza kuzitumia," alisema

Aidha Mkwasa amesema bado kazi kukiimarisha kikosi chake inaendelea lakini anaridhishwa na mwenendo wa timu mpaka sasa

"Mabadiliko yanaonekana, katika michezo ya nyuma hasa kipindi cha pili muda mwingi Yanga ilikuwa ikijilinda zaidi wakati mchezo ukiwa unaelekea mwishoni"

"Lakini jambo hilo halipo sasa, vijana wanajitahidi kucheza mpira muda wote na ndio maana leo wameweza kufunga mabao kwenye dakika za majeruhi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’