Dirisha dogo la usajili kwa msimu huu wa 2019/20 litafunguliwa Disemba 16 2019 na kufungwa January 15 2019
Ilizoeleka dirisha hilo kufunguliwa Novemba 15 na kufungwa Disemba 15 lakini TFF imekuja na mabadiliko hayo
Dirisha la usajili litafunguliwa wakati ligi ikiwa imesimama kupisha michuano ya CECAFA Senior Challenge ambayo itafanyika nchini Uganda
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Disemba 01 mpaka Disemba 19
Hivyo baada ya kumalizika kwa michezo ya kalenda ya FIFA, timu zitacheza raundi moja au mbili kisha ligi kusimama tena kwa karibu wiki nne
Mechi ya Watani ni baada ya dirisha dogo
Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa January 04 2020, wiki chache baada ya dirisha dogo kufunguliwa
Kwa maana hiyo nyota wapya watakaosajiliwa na timu hizo, watakaribishwa na mchezo wa watani wa jadi