Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesisitiza kuwa mpango walionao sasa ni kuhakikisha wanakamilisha uwanja wa Kaunda haraka ili kuepukana na gharama za kukodi viwanja
Pamoja na kuwa na eneo kubwa Kibada Kigamboni ambalo walipewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda, Dk Msolla amesema bado hawajapata Mwekezaji wa kufanya nae kazi lakini akipatikana wanaweza kuanza ujenzi mara moja
"Kwa sasa tunashughulikia eneo la uwanja wetu wa Kaunda, tunataka kukamilisha ujenzi haraka ili tuepukane na gharama za kukodi viwanja, " amesema Dk Msolla
"Uwanja wa Kaunda ukikamilika utatupa faida nyingi, kwanza wachezaji wetu wataishi katika Hostel zetu na kufanya mazoezi hapo Jangwani hivyo kutupunguzia gharama kubwa tunazotumia kwa ajili ya Hostel na kukodi viwanja"
"Lakini pia tutakuwa na mpango wa kuwaruhusu mashabiki kushuhudia mazoezi kwa kulipa kiingilio mpango ambao utatuongezea mapato"
Yanga inaendelea na mchakato wa ukarabati wa uwanja huo huku Serikali kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paulo Makonda ikiwahakikishia kuwa itamaliza changamoto ya mafuriko eneo la Jangwani