Vijana wako tayari kuikabili JKT Tanzania - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2019
Vijana wako tayari kuikabili JKT Tanzania - Mkwasa

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi cha timu hiyo kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Uhuru

Mkwasa amesema pamoja na kufahamu wanakwenda kucheza na timu imara, wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo

Mkwasa ameeleza kuridhishwa na muitikio wa wachezaji katika mazoezi anayowapa hivyo kumpa matumaini ya kufanya vizuri

"Baada ya mazoezi ya leo, vijana wangu wako tayari kwa ajili ya mchezo"

"JKT Tanzania ni moja kati ya timu nzuri naamini utakuwa mchezo mzuri sana, vijana wapo tayari kimwili na kiakili kuwakabili wapinzani wetu na kuondoka na pointi tatu hapo kesho," amesema Mkwasa

Uongozi wa Yanga umetaja viingilio vya mchezo huo kuwa VIP ni Tsh 10,000/- wakati upande wa Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

Yanga kesho huenda ikarejesha huduma ya baadhi ya nyota wake ambao walikuwa majeruhi Lamine Moro, Mohammed Issa 'Banka' na Ally Ally

Ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho leo kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’