Pamoja na kutokuwa bora sana kwenye mchezo wa leo, Yanga imeweza kuondoka na alama zote tatu kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania
Ushindi huo unamaanisha wachezaji 'wamesepa' na kitita cha Tsh Milioni 10 zinazotolewa na kampuni ya GSM, moja ya wadhamini wa Yanga
Tangu GSM ianze kutoa motisha hiyo, Yanga imeweza kushinda michezo yote minne na hivyo kujikusanyia Tsh Milioni 40
Nadhani mafanikio ya hamasa hii yanaonekana, hakuna shaka kama itatolewa kwa mechi zote, hakuna namna Yanga itaukosa ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Fikra ya kila mchezaji sasa ni kupata ushindi, wakipambana dimbani kuhakikisha wanafanikisha hilo
Β
ADVERTISE HERE