Winga Yusufu Mhilu ameisaidia Kagera Sugar kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli Fc leo yeye akifunga moja ya mabao ya timu hiyo
Mhilu sasa amefikisha mabao matano msimu huu akiwa kinara wa mabao kwenye kikosi cha Kagera Sugar
Ukizungumzia mafanikio ya Kagera Sugar, Mhilu ni mmoja wa wachezaji wanaoibeba timu hiyo ambayo baada ya kushinda leo imeiondoa Simba kileleni mwa msimamo wa ligi
Zahera hakumuhitaji na kuamua kumtoa kwa mkopo, ni miongoni mwa makosa ya usajili ambayo aliyafanya Mcongomani huyo ambaye Yanga ilimuondoa mapema mwezi huu
Kwani hata wakati akiondolewa na kupelekwa Ndanda Fc kwa mkopo, Mhilu alikuwa miongoni mwa wachezaji walioibeba Yanga msimu wa 2017/18
ADVERTISE HERE