Baada ya mchezo dhidi ya Alliance Fc, ligi itasimama kupisha michuano ya CECAFA Chalenji ambayo itafanyika nchini Uganda kuanzia Disemba Mosi
Kulingana na ratiba ya Bodi ya Ligi, baada ya michuano ya CECAFA Chalenji kumalizika, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba January 04 2020
Lakini mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itaifuata Alliance Fc Novemba 29 jijini Mwanza kucheza moja ya mechi zake za viporo kabla ya baadhi ya wachezaji wake kwenda kujiunga na timu za Taifa kushiriki michuano hiyo
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema timu itaendelea na mazoezi kipindi chote cha mapumziko hayo
Aidha amesema watawajumisha kwenye kikosi baadhi ya nyota ambao wanataka kuwasajili dirisha dogo kujiridhisha na uwezo wao
cut"Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu baadae tutaendelea na program zetu za mazoezi. Hatuwezi kukaa tu kwa kuwa ligi imesimama kwa muda mrefu," Mkwasa aliiambia Yanga TV
"Mipango yetu ni kuwa tutatumia kipindi hicho kuimarisha timu yetu. Tutakuwa na mechi nyingi za kirafiki. Pia tutawaalika baadhi ya wachezaji ambao tunataka kuwasajili kujumuika nasi"
"Ni wakati ambao pia tutawapa nafasi wachezaji wetu wa timu ya vijana ambao naamini tutaendelea kuwatumia katika michezo yetu mbalimbali"