FT : Kagera Sugar 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2017
FT : Kagera Sugar 1-2 Yanga
Mchezo wa mzunguuko wa sita ligi kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Kagera Sugar dhidi ya Yanga umemalizika kwa mabingwa watetezi kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini.

Mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali uliishuhudia Yanga ikitawala kipindi cha kwanza kwa kucheza kandanda safi wakati wenyeji walizinduka katika kipindi cha pili.

Obrey Chirwa aliifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 40, akimalizia pasi murua ya Ibrahim Ajib.

Bao la pili la Yanga liliwekwa kimiani na nyota wa mchezo huo Ibrahim Ajib kwenye dakika ya 51 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Obrey Chirwa.

Dakika tatu baadae Jafari Kibaya aliifungia Kagera Sugar bao la kufutia machozi kwa mpira wa kichwa baada ya kukosa mawasiliano kwa walinzi wa kati Yondani, Dante pamoja na mlinda lango Youthe Rostand.

Matokeo hayo yameipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kufikisha alama 12 sawa na Azam FC iliyolazimishwa sare ya bao 1-1 ya Mwadui FC.

Aidha ushindani baina ya timu zinazoshiriki ligi kuu msimu huu umeendelea kudhihirika baada ya Yanga kuwa timu pekee iliyoshinda katika michezo mitano iliyopigwa leo.

IBRAHIM AJIB MIGOMBA! Huyu mtu anajua sana!

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’