Kwa wale wavurugaji wa mijadala na vinara wa kuandika matusi na lugha zisizo na staha humu ndani, yeyote anaweza kuripoti maandiko yao
Ni rahisi, unapokutana na 'comment' yenye matusi au lugha isiyo na staha unaweza kutoa taarifa na itaondolewa na mhusika atachukuliwa hatua ikiwemo kuzuiwa kuandika chochote
Unachotakiwa kufanya bonyeza ki-box chenye comment husika, usiachie mpaka ukurasa wa MENU ujitokeze
Kisha chagua 'Report Comment', fuata maelekezo yatakayofuata ili maoni yako yapokelewe
Utaratibu huu utamuwezesha kila Mwana Jangwani kuweza kudhibiti wale ambao wanaingia kwenye jukwaa hili kwa lengo la kuleta usumbufu
Wasumbufu wameendelea kuondolewa na kufungiwa akaunti zao ingawa tunafahamu ipo changamoto wakifungiwa, wanafungua akaunti nyingine
Lakini utaratibu huu wa kuripoti maandiko yao, unarahisisha kuwabaini kwa haraka kisha kuwafungia
Jukwaa hili ni kwa ajili ya mashabiki wa Yanga, ni bahati mbaya sana wenzetu wachache wanadhani ni jambo jema na ujanja kuvamia na kutoa lugha zizizo na staha humu ndani. Tumeweka utaratibu wa kuwabaini na sasa tutaanza kuwaweka hadharani majina yao halisi