Kikosi cha Yanga leo kimekamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa kesho Ijumaa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Leo jioni Yanga ilipata nafasi ya kujifua katika dimba hilo la Kirumba ambalo litatumika hapo kesho
Kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Charles Mkwasa amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo
Amesema kikosi kina ari na hakuna majeruhi yeyote miongoni mwa wachezaji 18 waliosafiri kwa ajili ya mchezo huo
Huo utakuwa mchezo wa tatu Mkwasa anaiongoza Yanga tangu akabidhiwe majukumu ya kuinoa timu hiyo Novemba 05
Tayari ameiongoza Yanga kushinda michezo dhidi ya Ndanda Fc na JKT Tanzania
ADVERTISE HERE