Kaseke wa Mkwasa ni moto wa kuotea mbali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Nov 2019
Kaseke wa Mkwasa ni moto wa kuotea mbali

Kwa sasa ukizungumzia wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga hutaacha kutaja jina la kiunga mshambuliaji Deus Kaseke

Tangu Mkwasa akabidhiwe majukumu ya kuinoa Yanga mapema mwezi huu, Kaseke amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza

Lakini muhimu zaidi, Kaseke amekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio inayopata Yanga sasa

Kwa kiasi kikubwa ushindi wa michezo miwili iliyopita, umepita katika miguu yake

Jana katika mchezo dhidi ya Alliance Fc ni juhudi zake zilizozaa bao la ushindi la Yanga lililowekwa kimiani kwa ufundi wa hali ya juu ya mshambuliaji David Molinga 'Falcao'

Mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania Kaseke alitoa pasi mbili za mabao pamoja na kusababisha mpira wa adhabu uliowekwa kimiani na David Molinga

Ni huyuhuyu Kaseke ambaye wakati wa Mwinyi Zahera hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Kama Zahera bado anafuatilia mechi za Yanga, atakuwa akijilaumu kwa nini hakuwa akimuamini kiungo huyu mwenye 'mapafu ya mbwa'

Kaseke na nahodha Msaidizi Juma Abdul ni wachezaji ambao wameonyesha utofauti mkubwa chini ya Mkwasa

Wameufanya upande wa kulia kuwa na madhara sana kwa timu pinzani kwani mabao mengi yanayofungwa yanapita upende huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’