Majeraha yalisababisha niongezeke uzito - Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2019
Majeraha yalisababisha niongezeke uzito - Abdul

Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul, ameweka wazi majeruhi yaliyomsababishia aongezeke kilo 12, ndio yalimwaribia akashindwa kufanya vizuri ndani ya klabu yake ya Yanga na timu ya taifa, lakini baada ya kurudishwa kwenye kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, amesisitiza gari ndio limewaka, lazima watamtaka.

Abdul aliyetangazwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2015-2016, akiwashinda Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na Shiza Kichuya alipokuwa Mtibwa Sugar, akapotea jumla na mpaka sasa anarudishwa timu ya taifa na Kocha Mrundi Etienne Ndayiragije, imepita miaka minne.

“ Kitu kikubwa ambacho kilinipoteza kwenye soka ni kwa sababu ya maumivu. Nilikuwa kwenye majeruhi kwa kipindi kirefu, niliporudi uzito mkubwa uliongezeka hivyo ikawa changamoto kubwa kupambania nafasi na wenzangu ambao niliwakuta wako tayari.”

Beki huyo alisema, aliongezeka kilo 12, alipokuwa fiti alikuwa na kati ya 64 na 65 na aliporudi kutoka kwenye majeruhi, alikuwa na 76 ambazo kwa sasa amezikamua na kurudi kwenye hali yake.

"Majeraha na uzito ndio sababu kubwa iliyonipoteza mimi kwenye ramani ya soka na baada ya kuligundua hilo, nilipofanyia kazi, nimerudi kwenye hali yangu,” alisema Abdul.

“Ukiachana na changamoto hizo, kwenye kazi mimi najiamini ni mchezaji mzuri. Ninachotakiwa ni kufanya mazoezi na kucheza kwa bidii ili niweze kuisaidia timu na mimi mwenyewe.

“Nashukuru mwalimu kuona uwezo wangu na kuniita kwenye kikosi chake, upande wangu sitamwangusha, namwahidi yeye pamoja na Watanzania wote ni mapambano na kuwapa raha wanayohitaji, kikubwa ushirikiano”.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’