Mexime ni suala la muda Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2019
Mexime ni suala la muda Yanga

Uongozi wa Yanga umeanza mchakato wa kumnasa kocha wa Kagera Sugar Meckie Mexime ili kumuongeza kwenye benchi la ufundi kama Kocha Msaidizi

Mexime ambaye kwa sasa yuko mapumziko mkoani Morogoro baada ya ligi kusimama kupisha michuano ya Chalenji, amekiri kuzungumza na mabosi hao wa Yanga lakini bado hawajafikia mwafaka

"Ni kweli viongozi wa Yanga walinitafuta, lakini bado tunazungumza kama tutakubaliana nitakuja Dar es salaam kukamilisha masuala mengine," amesema

Yanga imedhamiria kuimarisha benchi la ufundi kabla ya mchezo dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa January 04 2020

Yanga na Simba ni kama 'mapacha' kwani wakati mwingine zimechukua maamuzi yanayofanana

Zote zilitimua makocha mwezi uliopita na wakati Yanga ikiwa mbioni kumnasa Mexime, klabu ya Simba imemchukua Selemani Matola aliyekuwa Polisi Tanzania kuwa kocha wao Msaidizi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’