Ajib, Chirwa wanaweza kumpa mafanikio Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Oct 2017
Ajib, Chirwa wanaweza kumpa mafanikio Lwandamina
Mabingwa mara tatu mfululizo ligi kuu ya Vodacom, Yanga wameweka kambi ya muda mkoani Tabora kujiandaa kuelekea Shinyanga kucheza na Stand United Oktoba 22.

Akili ya kocha wa timu hiyo, George Lwandamina kwenye matumizi ya Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu imekubalika na wakuu wake wa kazi.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-1 Lwandamina aliwatumia Ajib na Chirwa kama washambuliaji wa kati na wawili hao kuonyesha uwezo mkubwa wakifanya mambo mawili muhimu yanayofanana.

Chirwa ndiye aliyefunga bao la kwanza kwa timu yake lakini pasi ya bao hilo ilitengenezwa kifundi na Ajib iliyowafanya mabeki wa Kagera kupotea akitumia mguu wake wa kulia huku Chirwa naye akimalizia kwa mguu kama huo.

Ajib naye alifunga bao la pili katika kipindi cha pili kwa akili kama hiyo akipiga shuti la hesabu lililokwenda nyavu ndogo akitumia mguu wake wa kulia lakini pasi ya bao hilo ilitengenezwa na Chirwa akitumia mguu wa kulia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga Hussien Nyika amesema; "Nimefurahishwa na safu ya ushambuliaji hii ya Chirwa na Ajib unajua hawa wote wana akili nyingi sasa nilivyoona mimi kama wataendelea kucheza pamoja watakuwa hatari zaidi. Ndicho tunachokitaka."

Yanga kesho Jumatano itashuka katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuwavaa wenyeji wao Rhino ya hapa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu hiyo ya daraja la kwanza.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’