Beki wa kulia wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer' leo ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje tangu mwezi Agosti mwaka huu
Katika mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo, Boxer alishiriki lakini akianza na mazoezi maalum
Yanga sasa imebaki na majeruhi mmoja tu wa muda mrefu Juma Mahadhi ambaye nae huenda akaanza kuonekana dimbani mwezo ujao
Yanga leo imeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kombe la FA na mechi nyingine za ligi
Mabingwa hao wa kihistoria kesho Alhamisi wanatarajiwa kuelekea mkoani Kigoma
ADVERTISE HERE