Usajili wa Tariq ni mwanzo tu - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2019
Usajili wa Tariq ni mwanzo tu - Dk Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema usajili wa mshambuliaji Tariq Seif Kiakala ni mwanzo tu, kwani wanatarajia kusajili nyota wengine kulingana na mapendekezo yaliyotolewa

Akizungumza mapema leo wakati wa utambulisho wa mshambuliaji huyo, Dk Msolla alisema pamoja na changamoto ambazo timu inapitia, watahakikisha wanakiboresha kikosi chao ili kiwape furaha mashabiki

"Kuna maeneo kadhaa ambayo wadau wetu mmetoa maoni kuwa yanahitaji kuboreshwa. Tumeanza na Tariq, huu ni mwanzo tu kwani tumejipanga kuboresha sehemu zote zenye mapungufu," amesema

"Tunawaomba mashabiki wampokee na kumpa ushirikiano Tariq, sisi viongozi tutampa ushirikiano ili kuhakikisha tunatimiza malengo tuliyojiwekea"

"Tariq ni mchezaji mzuri kwa wale wafuatiliaji wa soka la Tanzania, jina lake sio geni kwani amewahi kutamba vilabu vya Stand United na Biashara United kabla ya kwenda Misri kujaribu bahati yake"

Utambulisho wa mshambuliaji huyo ulirushwa 'mbashara' na Azam TV, utaratibu ambao uongozi wa Yanga umeahidi kuendelea kuutumia kwa nyota wengine watakaosajiliwa

Mshambuliaji huyo huenda akasafiri leo kuelekea mkoani Kigoma kuungana na kikosi cha Yanga ambacho leo kinashuka dimbani kuumana na Mwamgongo Fc

Tariq anaweza kuwahi mchezo wa Jumapili ambao ni dhidi ya Mbao Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
35m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’