Mshambuliaji mpya wa Yanga Tariq Seif Kiakala amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa mapokezi waliyompa baada ya kukamilisha usajili wake kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria
Tariq amesema ni heshima kubwa kwake kujiunga na Yanga, anaamini kwa ushirikiano na wachezaji walipo, wataweza kutimiza malengo yliyowekwa na timu
"Juzi baada ya kukamilisha zoezi la kusaini mkataba wa kujiunga Yanga, sikupata nafasi ya kuwashukuru mashabiki wa timu yangu mpya. Hivyo nachukua fursa hii kuwashukuru kwa dua zenu mpaka hili limekamilika na nawaahidi sitawaangusha"
"Nitajituma na kushirikiana na wachezaji wenzangu kufikia malengo yaliyowekwa na uongozi wa klabu, najua mashabiki wote mtatuunga mkono mimi na wenzangu ili tuwape furaha," amesema
Tariq ameongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga baada ya timu hiyo kuvunja mikataba ya Sadney Urikhob na Juma Balinya
Kama TFF itamuidhinisha mapema huenda akaanza kuonekana dimbani wiki ijayo kwenye wa kombe la FA dhidi ya Iringa United