SMG afurahia mechi za kirafiki Kigoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Dec 2019
SMG afurahia mechi za kirafiki Kigoma

Kaimu Kocha Msaidizi wa Yanga Said Maulid 'SMG' amesema michezo ya kirafiki waliyocheza mkoani Kigoma imewapa mazoezi mazuri

Katika michezo hiyo ambayo Yanga ilicheza dhidi ya Namgongo Fc na Kigoma United, timu iliibuka na ushindi wa 2-1 na 3-0

"Tulicheza na timu ambazo mifumo tofauti. Mchezo wa kwanza ulikuwa na mbinu zaidi wakati mchezo wa pili ulikuwa wa nguvu," amesema

"Tumeweza kupata matokeo, tunarejea jijini Dar es salaam kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa FA dhidi ya Iringa United"

Mchezo wa pili dhidi ya Kigoma United uligubikwa na matukio ya kibabe ambapo mlinda lango Ramadhani Kabwili alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupigana na mchezaji wa Kigoma United

Beki Jaffar Mohammed alilazimika kumalizia dakika zilizokuwa zimebaki akiwa mlinda lango

Kwenye ziara ya mkoani Kigoma, Yanga iliwakosa baadhi ya nyota wake waliokuwa timu za Taifa za Tanzania Bara(3) na Zanzibar Heroes(4)

Pia iliwakosa baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao walichelewa kufika mkoani humo

Yanga inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Iringa United ambao utapigwa Disemba 21 kwenye uwanja wa Uhuru

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’