Timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeiaga michuano ya Chalenji baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uganda kwenye mchezo wa nusu fainali
Bao la mshambuliaji Fahad Bayo alilofunga kwenye dakika ya 86 liliihakikishia Uganda Cranes kutinga fainali ya michuano hiyo ambapo mchezo wa fainali watacheza na Eritrea
Elitrea iliilaza Kenya mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali


Matokeo hayo yamefuta matumaini ya Stars kuondoka na kitita cha Tsh Milioni 100 walichoahidiwa na Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' kama wangetwaa ubingwa wa michuano hiyo

Pichani : Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Juma Balinya alikuwa miongoni mwa mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo
ADVERTISE HERE