Funga kazi ya usajili bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2019
Funga kazi ya usajili bado

Baada ya kufanikiwa kuwasajili nyota karibu wote waliokuwa wakiwawania, bado Yanga hawajamaliza kazi

Inaelezwa bado nyota wawili wa kigeni huenda wakatua Jangwani kabla ya Jumanne ijayo

Nahodha wa UD Songo, kiungo mshambuliaji Luis Miquissone anaweza kuwa mmoja wao

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ameuita usajili huo wa mwisho ni FUNGA KAZI

"Karibu tena fundi Haruna Niyonzima sasa inakuja FungaKazi, " Bumbuli alimkaribisha kiungo mpya wa timu hiyo Haruna Niyonzima

Lakini pia inaelezwa Yanga inaweza kumshusha mshambuliaji Ghislain Yikpe Gnamien raia wa Ivory Coast aliyekuwa akiitumikia Gor Mahia kabla ya kuvunja mkataba wake hivi karibuni

Michakato yote hiyo inasimamiwa na kampuni ya GSM, wadhamini wa mabingwa hao wa kihistoria ambao wamejitosa 'mazima' kuisuka upya Yanga

Lengo kuu ni kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa msimu huu, huu ni mwanzo wa uwekezaji ambao GSM wanakwenda kuweka Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’