Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Patrick Aussems ni miongoni mwa makocha walioomba nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga
Aussems aliondoka klabu ya Simba mwezi uliopita baada ya uongozi wa timu hiyo kufikia uamuzi wa kumfuta kazi
Tetesi zinazomuhusisha kutua Yanga zilianza kushika kasi jana, hatimaye leo uongozi wa Yanga umetoa ufafanuzi kuhusu ukweli wa suala hilo
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Aussems ametuma CV zake akiomba nafasi hiyo inayokaimiwa na kocha Charles Mkwasa
"Kocha Aussems ni miongoni mwa waliotuma maombi kuwania nafasi ya kuwa kocha Mkuu wa Yanga. Hivyo ni jukumu la Kamati ya Ufundi kuamua, kama wataona anafaa basi tutaingia nae kandarasi," amesema
Katika hatua nyingine, Bumbuli amesema usajili unaofanywa na Yanga sio kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa January 04 2020
Amesema usajili huo unalenga kuboresha nafasi ambazo zilionekana kuwa na mapungufu
Bumbuli ameongeza kuwa wachezaji wote wanaosajiliwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa nyota wanne, Haruna Niyonzima, Tariq Seif, Ditram Nchimbi na Adeyum Saleh