Kikosi cha mabingwa kihistoria Tanzania Yanga kiko mkoani Mbeya ambapo jioni ya leo Jumanne, Disemba 24 2019 watashuka katika uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City ukiwa ni mchezo wa ligi
Msafara wa wachezaji 20 wa Yanga pamoja na benchi la ufundi waliwasili Mbeya mapema jana, jioni wakipata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Sokoine kuelekea mchezo huo
Ni mchezo ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Kwenye mchezo huo beki mpya wa Yanga Adeyum Saleh huenda akapata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza akiwa katika uzi wa Yanga baada ya TFF kutoa idhidni kwa wachezaji waliokamilisha usajili wa dirisha dogo na wana 'release letter' waruhusiwe kucheza
Nyota wengine wapya huenda wakaanza kuonekana katika michezo ijayo pale michakato yao hasa vibali kwa wachezaji wa kigeni itakapokuwa imekamilika