Mshambuliaji raia wa Ivory Coast Yikpe Gnamien alifanyiwa vipimo vya afya jana tayari kujiunga na Yanga baada ya makubaliano kufikiwa
Awali Yanga ilipendekeza mshambuliaji huyo kufanyiwa majaribio lakini suala hilo lilileta sintofahamu miongoni mwa wadau huku mwenyewe akigoma
Uongozi wa Yanga umesema lilikuwa ni sauala la kujiridhisha na uwezo wake hasa ikizingatiwa kuwa mabingwa hao wa kihistoria wamepata hasara msimu huu baada ya kulazimika kuvunja mikataba ya baadhi ya nyota wa kigeni ambao wameshindwa kutamba
Gnamien amefuzu vipimo vya afya na leo ataungana na timu mkoani Mbeya ambapo ataanza mazoezi wakati akisubiri tararibu nyingine za kukamilisha usajili wake zikae sawa
Mshambuliaji huyo alijiunga na Gor Mahia mwezi Julai 2019 kuchukua nafasi ya Jacques Tuyisenge aliyetimkia nchini Angola
Hata hivyo ameichezea timu hiyo kwa miezi minne tu na kuamua kuvunja mkataba wake baada mabingwa hao wa Kenya kushindwa kumlipa mishahara kutokana na ukata unaowakabili