Vita ya namba safu ya kiungo Yanga usipime

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2019
Vita ya namba safu ya kiungo Yanga usipime

Yanga imezidi kuimarisha safu yake ya kiungo baada ya kumsajili Haruna Niyonzima 'Fabregas' kutoka AS Kigali ya Rwanda

Ujio wa Niyonzima umeongeza vita ya namba katika safu ya kiungo

Kwani atawakuta viungo wengine wakiongozwa na nahodha Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Raphael Daudi na kiraka Said Juma 'Makapu'

Ni wazi Niyonzima ataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza, pengine atacheza sambamba na Tshishimbi na Balama

Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwa Fei Toto lakini msimu huu anaonekana kucheza chini ya kiwango

Pengine ujio wa fundi Niyonzima utamfanya ajitathmini na kurejesha makali yake

Kwani Fei Toto ni aina ya kiungo ambaye angeweza kutengeneza pacha nzuri zaidi na Niyonzima

Banka alikuwa na mchango mwanzoni mwa msimu kabla ya kupata majeraha wakati Bui alikuwa mchezaji wa kutegemewa wakati wa kocha Mwinyi Zahera

Lakini ni dhahiri wakati huu wa Mkwasa atahitaji kufanya kazi ya ziada ili kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwani Mkwasa amemrejesha Tshishimbi nafasi ya kiungo cha ukabaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’