Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema hawatabeba televisheni mbele ya waandishi wa habari kuonyesha uonevu wanaofanyiwa na waamuzi
Lakini anaamini itafika wakati mashabiki watachoshwa na uonevu wanaofanyiwa
Bumbuli ametoa maoni yake baada ya mchezo wa jana kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Sokoine na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
"Hatutabeba TV kwenda nazo kwenye Press Conference. Unfair business, unfair decisions. Kuna siku wananchi wataamua," ameandika Bumbuli kwenye ukurasa wake wa mtandao Instagram
Tukio la kubeba TV mbele ya waandishi wa habari liliwahi kufanywa na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara mwaka 2016 akitumia njia hiyo kufikisha malalamiko ya uonevu waliodai kufanyiwa na waamuzi kwenye mechi zao wakati huo