Stand United yatamba kuiduwaza Yanga Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
20 Oct 2017
Stand United yatamba kuiduwaza Yanga Jumapili
Stand United itajaribu kurudia rekodi nzuri dhidi ya Yanga Jumapili hii kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Msimu uliopita Yanga kwa mara ya kwanza ilikubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja huo shukrani kwa bao la Pastory Atanas ambaye kwa sasa yupo Singida United.

Hivyo mchezo wa Jumapili utakuwa mgumu kwa timu zote mbili kwani Yanga wanataka kulipiza kisasi cha msimu uliopita na kujiweka vizuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Stand United wanataka kupata ushindi ili kujinasua mkiani kwani mpaka saa wana pointi nne huku wakiwa katika nafasi ya 15.

Kocha Msaidizi wa Stand United, Agustino Malindi alisema watawashangaza Yanga kama walivyofanya msimu uliopita kwa kuwa kikosi chao kimeimarika siyo kile kilichoanza Ligi.

Alisema walisajili wachezaji damu changa ambao mwanzoni walikuja hawajazoea ligi, lakini sasa wameimarika hivyo lazima mchezo huo wanyakuwa pointi tatu.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema wao wako tayari kwa mechi zote za Ligi kuu katika mzunguko wa kwanza kwani mipango yao ni kutaka kutetea ubingwa

“Tuko tayari kutetea ubingwa wetu hivyo tumejipanga kwa mechi zote kuweza kupata ushindi hatuangalii mchezo mmoja mmoja,”amesema Nsajigwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →