Ushindi kuipaisha Yanga hadi nafasi ya tatu msimamo VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2019
Ushindi kuipaisha Yanga hadi nafasi ya tatu msimamo VPL

Jioni ya leo Ijumaa, Disemba 27 2019 kikosi cha Yanga kitakuwa mkoani Iringa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Mchezo huo awali ulipaswa kupigwa mkoani Mbeya lakini ulihamishwa baada ya uwanja wa Sokoine 'kuvurugwa' kwenye Tamasha la Muziki la Wasafi juzi

Mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa Yanga kwani mpaka sasa Tanzania Prisons ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu

Tanzania Prisons inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 20 wakati Yanga wanashika nafasi ya 10 wakiwa na alama 18

Hata hivyo ushindi kwa Yanga utawawezesha mabingwa hao wa kihistoria 'kuchupa' mpaka nafasi ya tatu

Aidha baada ya kukosa ushindi katika michezo miwili iliyopita, mchezo huu ni muhimu kwa Yanga kuondoka na alama zote tatu

Yanga walifanya mazoezi ya mwisho jana mkoani Mbeya kisha kuondoka usiku kuelekea Iringa tayari kwa mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’