Kiungo Issa Bigirimana 'Walcott' amerejea kwao Rwanda baada ya kuvunja mkaraba wake na Yanga
Bigirimana aliyetua Yanga akitokea klabu ya APR, mashabiki walikuwa na matumaini makubwa kwake
Hata hivyo nyota huyo alishindwa kutamba akicheza chini ya dakika 20 mechi zote za mashindano
Bigiriamana alikumbana na changamoto ya majeraha ya mara kwa mara tangu alipojiunga na Yanga mwezi Juni
Nyota huyo alianza kusumbuliwa na majeraha mapema tu wakati Yanga ikiwa imeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na msimu
Kukosekana uwanjani mara kwa mra pengine kulimfanya apoteze kujiamini na kushindwa kupata nafasi ya kucheza hata pale alipokuwa 'fit'
Ni wazi Bigirimana 'alipima upepo'na kuona hatakuwa na nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kocha Charles Mkwasa ambaye anapenda wachezaji wanaojituma
Bigirimana anakuwa mchezaji wa tatu wa kigeni kuvunja mkataba na Yanga baada ya kushindwa kuonyesha makali
Ikumbukwe pia wachezaji hawa walikuwa wakibanwa katika mikataba yao kuwa kama hawatafanya vizuri Yanga ingeweza kuchukua hatua dhidi yao
Kwa sasa Yanga inasaka mchezaji mwingine wa kigeni atakayechukua nafasi yake
Luis Miquissone wa UD Songo ndiye aliyekuwa chaguo la kwanza lakini usajili wake unaonekana kuwa mgumu
Taarifa za ndani zinabainisha kuwa Yanga sasa inamuwania Orebotse Mongae wa Baroka FC
Mhandisi Hersi Saidi, Mkurugenzi wa GSM ambaye alikwenda Afrika Kusini kukamilisha usajili wa Miquissone, anaweza kurejea na Mongae