Kampuni ya GSM imeahidi kumzawadia godoro chapa GSM mchezaji wa Yanga atakayeibuka nyota wa mchezo kwenye pambano la watani wa jadi Januari 04 2020
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Matina Nkurlu amesema wanaamini zawadi hiyo itawapa motisha wachezaji na kuwaongezea morali ya kupambana
Pia ametoa wito kwa wapenzi wa Yanga kujitokeza kwa wingi na kununua jezi za timu yao ili wakaiunge mkono kumua mnyama siku hiyo kwani inawezekana.
"Tunaamini zawadi hii itawaongezea wachezaji morali ya kupambana kuiwezesha Yanga kupata ushindi na hivyo kuwapa raha mashabiki wao na kuendelea kupata matokeo chanya kwa mechi zingine zijazo," alisema Nkurlu.
"Yanga ni klabu kubwa na bora hapa nchini kama ilivyo kwa magodoro yetu Chapa GSM hivyo mashabiki wao nao wanastahili matokeo yaliyo bora uwanjani ndio maana tumeamua kutoa zawadi ili kuwapandisha mzuka wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo huo muhimu wa Jumamosi ya Januari 4."