Simba na Mtibwa zimeendelea kukabana koo kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kupata ushindi katika michezo yao ya mzunguuko wa saba iliyopigwa leo.
Simba imeichapa Njombe Mji mabao 4-0 wakati Mtibwa Sugar imeilaza Tanzania Prisons bao 1-0.
Timu zote zimefikisha alama 15 lakini Simba imezidi kujichimbia kileleni kwa tofauti ya mabao ikiwa imefunga mabao 19 na kufungwa manne.
Yanga itashuka dimbani kesho Jumapili ugenini mkoani Shinyanga kuumana na Stand United.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu lakini Yanga inahitaji kuibuka na ushindi ili kuweka morali ya wachezaji juu kabla ya mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba wiki ijayo.
Matokeo tofauti na ushindi yatashusha morali ya wachezaji na hata mashabiki waliorejesha imani kwa timu yao baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Azam FC na Singida United nazo zimeendelea kukumbwa na wakati mgumu ugenini baada ya kulazimishwa suluhu katika michezo yao ya leo.

ADVERTISE HERE