Kuelekea mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, mashabiki wa Yanga kundi la YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO, wamezindua 'band' ya uhamasishaji ambayo itakuwa na jukumu la kuongeza hamasa uwanjani katika michezo ya Yanga
Kiongozi wa kundi hilo Muddy Kabwe amesema kupitia band hiyo wataongeza hamasa kwa mashabiki uwanjani wakati timu inapokuwa ikicheza
Kabwe amesema uzinduzi wa kikundi hicho ni mwanzo tu, kuna mambo mengine makubwa wanakusudia kuyafanya kwa ajili ya kuiunga mkono Yanga
ADVERTISE HERE