Nyota watano waliosajiliwa na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo wamepata vibali na wanaweza kushiriki mchezo dhidi ya Simba hapo kesho
Baada ya kufanikiwa kupata leseni za wachezaji wazawa, Adeyum Saleh, Tariq Seif na Ditram Nchimbi, ITC za wachezaji wa kigeni Haruna Niyonzima na Yikpe Gnamien nazo zimewasili
Kwa maana hiyo Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kazi itabaki kwake kuamua nani aanze
Ukimuondoa Niyonzima ambaye aliwasili jana, wachezaji wengine wamefanya mazoezi na timu kwa angalau wiki moja au zaidi hivyo wako tayari kwa mchezo huo
Β
ADVERTISE HERE