Nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi kuwaunga mkono katika mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Abdul amesema mashabiki hawana sababu ya kuwa na wasiwasi kwani timu yao imejiandaa kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo huo
Aidha, Abdul amewatahadharisha mashabiki wa Simba kuwa wasiende uwanjani na matokeo mfukoni kwani jambo lolote linaweza kutokea
"Nawaambia mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani, wasitishwe na tambo za Manara na mashabiki wa Simba kwani sisi tumejiandaa sawasawa"
"Ni mchezo ambao tumepania kuibuka na ushindi. Tunawapa tahadhari mashabiki wa Simba kuwa wasiingie uwanjani na matokeo kwani mambo yanaweza kuwa tofauti"
"Mpira ni mchezo wa makosa, yule atakayefanya makosa ataadhibiwa, " alisema Abdul