Lunyamila, Mmachinga waongeza mzuka kwa wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2020
Lunyamila, Mmachinga waongeza mzuka kwa wachezaji

Wachezaji wa zamani wa Yanga Edibily Jonas Lunyamila na Mohammed Hussein 'Mmachinga' walipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji kuwapa uzoefu wao wa mechi za dabi huku wakiwataka wahakikishe wanashinda mchezo wa leo

Nyota hao ambao historia yao Yanga inaweza kuandikwa kwa wino wa dhahabu, amesema mchezo dhidi ya Simba leo unaweza kuwa mwepesi kuliko wengi wanavyofikiria

Amewataka wachezaji kuwa watulivu na wafahamu kuwa ni heshima kubwa kwao kushiriki mchezo huo na matokeo mazuri yatakuwa kumbukumbu ambayo itabaki kwa miaka mingi

"Mchezo dhidi ya Simba hautakuwa mgumu kwenu, mnapaswa kuwa watulivu na mfahamu ni heshima kubwa kucheza mchezo huu hasa ukiwa mchezaji wa Yanga"

"Hakuna kitu wanataka mashabiki wa Yanga kutoka kwenu zaidi ya ushindi. Mkifanya vizuri, mtanufaika kiuchumi lakini pia ni heshima kwenu, mtabaki kwenye mioyo ya mashabiki wenu kwa miaka mingi," alisema

Nae Mmachinga aliwataka wachezaji kutoka na hofu kwani mchezo wa leo ni wa kawaida

"Tuna kikosi kizuri, wala msiwe na hofu, chezeni kama mlivyoelekezwa na Mwalimu, hawa ni wetu tu"

GSM, wadhamini wa Yanga wameweka mezani kitita cha Tsh Milioni 50 kwa ajili ya ushindi dhidi ya Simba leo

Lakini mchezaji bora wa mchezo kwa upande wa Yanga pia atazawadiwa godoro 'brand" chapa GSM

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’