Mkwasa kuamua matokeo ya Yanga leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2020
Mkwasa kuamua matokeo ya Yanga leo

Silaha kubwa leo kwenye mchezo dhidi ya Simba ni safu ya kiungo. Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa atatilia mkazo safu hiyo

Ni kutokana na ukweli kuwa ubora wa Simba hutegemea zaidi safu yake ya kiungo

Bila shaka Mkwasa leo atapanga viungo wengi ili kuhakikisha anatawala sehemu hiyo

Mkwasa anaweza kuwapanga Mapinduzi Balama/Niyonzima, Papy Tshishimbi na Abdulaziz Makame kama viungo watatu iwapo atatumia mfumo wa 4-3-3

Kaseke na Patrick Sibomana huenda wakatokea pembeni wakati Ditram Nchimbi, David Molinga au Yikpe Gnamien mmoja wao anaweza kuanza mshambuliaji wa kati

Yanga haina wasiwasi sana kwenye safu yake ya ulinzi licha ya kumkosa Lamine Moro anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano

Mkongwe Kelvin Yondani na Ally Mtoni wanapewa nafasi ya kuanza wakiwa mabeki wa kati wakati Adeyum Saleh na Mustafa Suleyman au Juma Abdul wanaweza kucheza pembeni

Langoni huenda akarejea Farouk Shikhalo ambaye hakucheza michezo miwili iliyopita akimpisha Metacha Mnata

Kikubwa katika mchezo wa leo, Mkwasa anahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kukaba, lakini pia kwenye safu ya ushambuliaji atahitaji wachezaji wenye kasi

Safu ya ulinzi ya Simba haina wachezaji wenye kasi hivyo mara nyingi wanaposhambuliwa kwa kushitukiza uwezekano wa kuwafunga ni mkubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’