FT : Stand 0-4 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2017
FT : Stand 0-4 Yanga
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Yanga, leo wametoa onyo kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo baada ya kuwafumua Stand United mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Licha ya kupata ushindi huo muhimu, Yanga pia ilionyesha kandanda safi kwa kucheza soka la kasi kupitia mashambulizi ya pembeni.

Ibrahim Ajib ameendelea kudhihirisha ubora wake ambapo leo amepachika mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao matano.



Moja ya mabao yake ulikuwa mpira wa adhabu alioupiga pembeni karibu na kibendera cha kona kwenye dakika ya 23. Bao hilo linafanana kabisa na bao alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji.

Kwa mara nyingine uelewano wake na Obrey Chirwa ulizaa bao la pili kwenye dakika ya 34 ambapo Ajib aliutumbukiza mpira wavuni baada ya kutengewa pasi murua na Chirwa.

Yanga ikiwatumia Papi Kabamba Tshishimbi na Pato Ngonyani ilitawala sehemu ya kiungo na kuwapa wakati mgumu viungo wa Stand United na kuilazimu timu hiyo kutumia mipira ya mirefu.

Hata hivyo safu ya ulinzi ya Yanga leo iliyokuwa chini ya nahodha Nadir Haroub Cannavaro na Andrew Vicent 'Dante' ilikuwa imara kuondoa hatari zote langoni.

Kwenye dakika ya 53 Pius Buswita akaifungia Yanga bao la tatu kwa kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Ajib kabla Chirwa hajafunga bao la nne kwenye dakika ya 69 akitumia makosa ya mlinda lango aliyeshindwa kuwahi mpira uliokuwa umepigwa na Buswita.

Katika dakika 15 za mwisho kocha Lwandamina aliwatoa Chirwa, Ajib na Mwashiuya na kuwapa nafasi Said Mussa, Emanuel Martin na Yusuph Mhilu.

Kwa kandanda iliyoonyeshwa na vijana wa Yanga leo ni dhahiri sasa wako tayari kuubakisha ubingwa wa VPL Jangwani kwa msimu wa nne mfululizo.

Aidha Yanga iko tayari kwa mchezo dhidi ya Simba wiki ijayo, oktoba 28.

Ushindi dhidi ya Stand umeirudisha Yanga kwenye nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 15 sawa na Simba na Mtibwa Sugar.

Sasa Yanga imefunga mabao 10 na kuruhusu mabao matatu hivyo kuwa na tofauti ya mabao saba.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’