Banka aahidi kuendeleza moto wa mabao Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jan 2020
Banka aahidi kuendeleza moto wa mabao Zanzibar

Wakati akitarajiwa kuibeba tena timu yake itakaposhuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar leo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mohamed Issa 'Banka', ametoa siri ya kuendelea kucheka na nyavu

Banka amefunga mfululizo wakati huu akitokea chumba cha majeruhi, ambapo kabla ya juzi kutupia dhidi ya Jamhuri kwenye mechi ya Kombe la Mapinduzi, pia alifunga dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Katika mechi hiyo ya juzi iliyopigwa Uwanja wa Amaan na Yanga kushinda 2-0, Banka alitokea benchi kipindi cha pili na kutupia dakika ya 85 baada ya Adeyum Saleh kutangulia kuziona nyavu dakika ya 45.

Kiungo huyo fundi amewataka mashabiki wa Yanga kufurahia matunda yake baada ya kumvumilia kipindi akiwa majeruhi.

"Siri kubwa ya mafanikio haya ni mazoezi na kujituma, lakini pia ushirikiano mkubwa ninaopata kutoka kwa wachezaji wenzangu

"Nawaomba mashabiki wa Yanga waendelee kutuunga mkono watafurahia ubora wetu katika mechi zinazofuata," Banka alisema.

Akiuzungumzia mchezo wa nusu fainali leo dhidi ya Mtibwa Sugar, Banka amesema utakuwa mgumu kwa kuwa ni timu inayowafahamu vizuri.

"Mtibwa tunacheza nao ligi moja na ni timu bora, hautakuwa mchezo mwepesi, lakini tumekuja kupambana," alisema.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
54m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’