Sasa hii ndio Yanga tunayoifahamu!

Admin By Admin
β€’
23 Oct 2017
Sasa hii ndio Yanga tunayoifahamu!
Yanga imeondoka na alama zote sita kanda ya ziwa baada ya kushinda michezo yake yote miwili.

Jumapili iliyopita Yanga ilianza kwa kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 na leo kuilaza Stand United mabao 4-0.

Katika michezo yote miwili licha ya kuwa ugenini Yanga ilicheza kandanda la kuvutia huku ikitengeneza na kutumia ipasavyo nafasi za mabao.

Yanga hii ndio ile ambayo mashabiki walikuwa wakiililia. Na hakika benchi la ufundi linahitaji pongezi kwani matunda ya kazi yao yameanza kuonekana.

Uvumilivu wao umeanza kuzaa matunda, muhimu ni kuendelea kuwaunga mkono.

Tumeona sasa Yanga inaweza kucheza kwa dakika 90 bila kuchoka, vijana sasa wanapumzi na wana stamina ya hali ya juu.

Morali ya wachezaji iko juu na ushindani baina ya wachezaji umefanikisha kuwafanya wawe imara.

Wachezaji kama Pato Ngonyani na Nahodha Cannavaro hawakuwa wamecheza mchezo wowote wa ligi kabla ya leo, lakini wameonyesha viwango vizuri.

Kwa kasi hii, Oktoba 28 tunachinja mnyama pale Uhuru mapemaaa. Huko waliko wanafahamu na hofu itakuwa imewajaa.

Baada ya ushindi mnono leo msemaji wao amekosa la kusema anabaki kumshushia lawama mtangazi wa Azam TV aliyetangaza mabao ya Ajib!

Hivi kwa mabao yale alitaka mtangazaji atangazeje? Ndio, mabao mengi yanafungwa lakini mabao anayofunga Ajib yana upekee!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’