Nugaz afafanua kauli yake kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2020
Nugaz afafanua kauli yake kombe la Mapinduzi

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema Mashindano ya Mapinduzi yana historia kubwa katika maendeleo ya mpira wetu na kudumisha udugu na katu hawezi kuyadharau

Nugaz ametoa ufafanuzi kuhusu kauli  aliyoitoa juzi ambayo ilinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Yanga haikuwa imeweka mkazo kwenye mashindano hayo madogo ikihofia wachezaji wake kuumia

Jana msemaji wa Simba Haji Manara alikwenda mbali kwa kuita kauli hiyo kuwa ni dharau kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Nugaz ameomba radhi kwa wote waliokwazika lakini amesisitiza hawezi kuidharau Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

"Kwa watu wanaonifahamu mimi daima wanajua khulka yangu ya mapenzi na uzalendo kwa nchi yangu! Hakika,haitokuja siku mimi kuonyesha dharau kwa kwa vitu ama watu ninaowathamini, kuwapenda na kuwaenzi," ameandika Nugaz kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

"Nikiwa naifahamu vyema historia ya Mapinduzi yetu adhimu na kwa kutumia mitandao yangu ya kijamii na kazini,nimekuwa mmoja kati ya watu wanayoyathamini, kuyafurahia na kuyatangaza kwani yamekuwa mbegu bora ambayo leo tunajivunia kama Taifa moja"

"Mashindano ya Mapinduzi yana historia kubwa katika maendeleo ya mpira wetu na kudumisha udugu,siyo tu ndani yetu bali hata Afrika mashariki"

"Mashindano haya yanatutangaza na kutufanya tujivunie utu na heshma yetu. Nawaomba msifadhaishwe na kauli za watu wanaopotosha kauli yangu kwa ajili ya kutimiza matakwa ya"

"Naomba pia muniwie radhi kwa yeyote aliyedhikika na kauli ile,napenda muamini ya kuwa, heshima niliyonayo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein itaendelea kudumu daima na namuombea kila lenye kheri katika maadhimisho ya sherehe hizi"

"Mapinduzi Daima"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’