Ni Ajib kila kona

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2017
Ni Ajib kila kona
Ibrahim Ajib Migomba ameirudisha furaha ya mashabiki wa Yanga iliyoonekana kufifia mwanzoni mwa msimu.

Mabao yake matano yameivusha Yanga kutoka kwenye kipindi kigumu na sasa kuna kila dalili ya kicheko kwa kipindi chote kilichobaki kuelekea ubingwa wa nne mfululizo.

Mabao ya mkali huyo yamewapagawisha wengi mpaka wengine kuamini thamani yake unaweza hata ukaombea mkopo benki!

Aidha mafanikio yake ndani ya kikosi cha Yanga yamemuweka kwenye wakati mgumu kiungo Haruna Niyonzima aliyewahi kuwa kipenzi cha mashabiki wa Wana Jangwani kabla hajaamua kutimkia Simba msimu uliopita.

Kumekuwa na mlinganisho baina ya wachezaji hao wawili 'waliobadilishana' timu lakini ni Yanga inayonufaika zaidi na usajili wa Ajib.

Akiwa amenunuliwa Yanga kwa kadirio la Mil 50, Ajib tayari amepachika mabao matano ya kutengeneza mengine kadhaa.

Wakati upande wa Niyonzima mambo hayamuendei vizuri ndani ya kikosi cha Simba.

Licha ya kununuliwa kwa zaidi ya Mil 120, na kuwa mchezaji anayelipwa pesa ndefu zaidi katika kikosi cha Simba, bado hajafanikiwa kufunga wala kutengeneza bao lolote.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’