Yanga imeshindwa kutamba uwanja wa Uhuru baada ya kufumuliwa mabao 3-0 na Kagera Sugar
Kukosekana kwa umakini kumeigharimu Yanga leo na kujikuta ikipoteza mchezo ambao waliutawala dakika za mwanzo
Mabao mawili kati ya matatu ya Kagera Sugar yalitokana na makosa ya wachezaji wa Yanga wenyewe
Kadi nyekundu iliivuruga Yanga
Yanga ilipoteza mwelekeo kwenye dakika ya 39 baada ya kiungo Mohammed Issa kutolewa nje ikiwa ni matokeo ya kuonyeshwa kadi mbili za njano
Kipindi cha pili Yanga haikuweza kwendana na kasi ya Kagera Sugar ambao walitumia vyema wingi wao uwanjani
Ni mchezo ambao Yanga ingeweza kufungwa mabao mengi kama sio uhodari wa mlinda lango Faroukh Shikhalo aliyeokoa mabao ya wazi kwenye dakika za majeruhi
ADVERTISE HERE